Sunday, February 26, 2012
Friday, February 24, 2012
EAST AFRICAN GOSPEL STAR ROSE MUHANDO SIGNS MULTI-RECORD DEAL WITH SONY MUSIC

Wednesday, February 22, 2012
VOTE FOR IZZO B (KILI MUSIC AWARDS)

UJUMBE KUTOKA KWA MC GEORGE NA SHOW YA TMK WANAUME FAMILY KUFANYIKA MARCH 3 MBEZI LUISI!!
Niaje kiongozi? Tutakua na shoo yetu na TMK itakayofanyika Machi 3, pande za Mbezi Luis, Dar ndani ya Ukumbi wa Times Square. Kwa mara ya kwanza tangu niliporudi kwenye game mwaka jana nitasimama stejini siku hiyo kwa utambulisho wa ngoma zangu kama Hadithi iliyotoka mwaja juzi mwishoni, Narudi Nyumbani inayofanya vizuri hivi sasa na nyingine kibao. One Love m2 mzima.
ALICHOKISEMA JOSEPH MBILINYI KWA WATU WAKE BAADA YA MAPATANISHO

ASANTENI SANA...
Tuesday, February 21, 2012
WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AWAPATANISHA MBUNGE JOSEPH MBILINYI NA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS MEDIA GROUP
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.Monday, February 20, 2012
Vote For Roma - Mathematics

BEST HIPHOP ARTIST, Send P2 to 15747
BEST HIPHOP SONG, Send J3 to 15747
or Email the Code F4, P2, or J3 to
ktma@innovexdc.com
or vote also at
http://www.kilitime.co.tz
NEW TRACK: Bonta ft. Farida - MATUSI.
CAPTAIN TUNDA MAN, ANAOMBA KURA YAKO.
Mpigie kura Captain Tunda Man kwenye Kili Music Awards....Tuma neno V2 kwa njia ya sms kwenda namba 15747 au barua pepe ktma@innovexdc.com au www.kilitimetz.com kura yako ndio ushindi wake.
DYNA ANAOMBA KURA YAKO.
DIAMOND PLATINUM ANAOMBA KURA YAKO.

Kili B1
Kili C2
Kili F3
Kili R1
Kili U1
Kili V3
Kili V4... Na kila moja utume kwenda namba 15747 au kupitia http://www.kilitime.co.tz kumuzesha diamond kutwaa tunzo hizi za kili music awards..
SASA UNAWEZA KUCHAT NA PROF JAY KWA SMS MUDA WOWOTE ULE.

Frost toka TGP na Moplus Way Back

Sunday, February 19, 2012
Walioiga nyimbo kuporwa tuzo za Kili!
Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro imesema itamnyang'anya tuzo msanii atakayebainika kwamba wimbo uliompatia tuzo hizo aliuiga. Kauli hiyo ilitolewa na mmoja wa wanakamati hao, Innocent Nganyagwa katika semina ya wanamuziki wanaowania tuzo hizo iliyofanyika Alhamisi Dar es Salaam.
“Tukubaliane, tuzo zitatolewa, lakini baadae hata kama ni mwakani, kamati ikigundua kuwa msanii ‘ulicopy na ku-paste’ tutakunyang’anya tuzo, cheti kila kitu sijui upande wa pesa kama utakuwa ushazitumia au vipi,” alisema. Kauli hiyo ya Nganyagwa ilitokana na maoni yaliyoolewa na Prodyuza Man Water kwamba kuwe na tuzo ya ubunifu.
“Kuwe na tuzo ya Producer mbunifu basi, kwa sababu kuna wengine unaona kabisa kazi zao wameiba mahali, hapo msanii, Producer wanakuwa wamecopy na kupaste kazi ya mtu Fulani… hivi hawa kwanini wasipewe adhabu kali, hata kama ya kufungiwa kwa miaka miwili ikibidi,” alisema Man Water.
Akifafanua kwenye suala la ubunifu Man Water alisema kuwe na kipengele hicho ili kuwaibua maproduza wabunifu akitolea mfano wimbo wa Dushelele wa Ali Kiba ambao ameutengeneza yeye.
“Kwa mfano kama Dushelele ule ni ubunifu, hivi unaweza kuuweka kwenye mziki gani, ipo kama Rhumba kidogo, kisanola ya kina Koffie, na mahali popote unachezeka hata mtu akitaka kucheza kama taarab anaweza,”alisema.
“Lakini pia nasikitika sana watu wa Kili Academy wameuweka wimbo huu kushindana kwenye kipengele cha Afro Pop, Dushelele sio Afro Pop, mimi ningependa kutoa ushauri kama wanaokaa kwenye hiyo Academy kuchagua nyimbo za kushindana, wakishindwa kujua mziki Fulani upo kwenye mahadhi yepi basi watupigie simu tu tutawaambia kuliko kuushindanisha mziki katika kipengele ambacho sio”.
Aidha Man Water aliwaomba waandaaji kufikiria kutoa tuzo ya msanii anayeshindanishwa mara nyingi kwenye tuzo hizo. “Kwa mfano mimi sijawahi kupata tuzo, lakini kwa muda mrefu nimekuwa nikishindanishwa, maana yake pale kuna kitu ambacho mimi ninacho basi waandaaji watoe tuzo ya kutambua hilo,”alisema.
Thursday, February 16, 2012
TAMASHA LA KUONGEZA MAARIFA KUFANYIKA, MARCH 8, SIKU WANAWAKE DUNIANI JIJINI MWANZA, VICKY KAMATA KUTOA BURUDANI!!
Tamasha la kuongeza maarifa, linatarajiwa kufanyika machi 8 mwaka huu, ikiwa ni siku ya wanawake duniani.
Tamasha limeandaliwa na akina dada kutoka kundi la Bedefesera hapa jijini Mwanza na litafanyika kwenye hoteli iliyo na hadhi ya kimataifa ya Gold crest.
Unajua utapata maarifa gani siku hiyo? Karibu uungane, kwa kununua kadi yako ya Tsh 30,000/= itakayokuwezesha pia kupata chakula cha jioni na vinywaji laini. Piga simu namba 0683962902 kwa manunuzi ya kadi yako.
Bedefesera inaundwa na watangazaji mahiri hapa nchini, akiwemo Rahab fred, Beatrice Rabach, Felister Kulwijira, Deborah Mpagama, Erica Elias na Seda Ilija.
Akizungumza na Blog hii, Mwenyekiti wa kikundi hicho Rahab Fred, amesema Tamasha litatoa mafunzo ya Ujasiriamali, Malezi ya Familia, Afya na jinsi ya kuweza kupata mikopo kwa masharti nafuu.
Burudani kabambe inatarajiwa kutolewa na mbunge wa viti maalum kutoka Geita Mh. Vick Kamata, pamoja na wasanii wengine maarufu kibao
Kazi kwenu wadau kuhudhuria tamasha hilo, hakika Blog ya The Big Top Ten, inawatakia mafanikio mema katika mwanzo mzuri wa kuongeza maarifa kwa wanajamii...Bigup Bedefesera!!!!!






