Muhsin Mambo aka MC Stopper ndiye alikuwa MC wa shughuli yote ya bonanza hilo
Kutokana na Bonanza hilo kuwa la muhimu ilibidi kamera nyingi zitunmike, Huyu ni Fatma Shemweta akipiga picha matukio katika bonanza hilo.
Mchezo kama huo pia ulifanywa na kina dada wa kampuni hiyo kama hivi
Kwa kina dada waliokuwa kwenye bonanza hilo vivazi navyo vilishindana kama hivi
Hatimaye upande wa kushoto wakaibuka washindi wamchezo wa kujifurahisha wa kuvutana kwenye kamba
Upande wa Nape ukizidisha kasi ya kuwavuta wa upande wa pili ambao walianza kuanguka
Kuleni pozi basi: Fatma Shemweta aakiwaambia Mariam na Grory wakati akiwapiga picha
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kushoto) akishiriki mchezo wa kuvutana kwa kamba uliofanywa na wafanyakazi wa Sahara media group, mjini kwenye ufukwe wa ziwa Victoria jijini Mwanza leo. Upande wa Nape ulishinda.
Kina dada wa kampuni hiyo wakifurahia michezo
Baada ya kushiriki mchezo wa kuvutana kwa kamba Nape akizungumza mawili matatu na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Pamela na Mary.
Lakini Bonanza hilo likamkutanisha pia Nape Steven Mhozya (kulia) ambaye walisoma wote shule ya sekondari Nsumba jijini Mwanza miaka yab 90.
Nape na baadhi ya wachezaji wa mchezo wa kuvuta kamba waliokuwa upande wake, wakishangilia baada aya kuwashinda wenzao
0 comments:
Post a Comment